Chuo Kikuu cha Egerton
Jacqueline Kamau
A13/30196/08
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
Fasihi ,Lugha na Isimu
KISW 413; Tamthilia ya kisasa ya Kiswahili
Uchambuzi wa Tamthilia ya Kifo Kisimani
Mhadhiri; Bw.Daudi Chacha
25/04/ 2012
TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI
UTANGULIZI
Tamthilia ya
Kifo Kisimani
imeandikwa na kithaka wa Mberia. Toleo la kwanza la kitabu hiki
ililikuwa mwaka wa 2001 na kina chapa nyingi hadi kufikia mwaka wa
2009.kimechapishwa na Marimba Publications Ltd.
Anwani
Anwani huwa ni jina la kitabu.Mwandishi amefaulu kutumia anwani’Kifo
Kisimani’. Anwani hii inaashiria kifo cha Mwelusi pale kisimani
alipouliwa na Gege.
Pia anwani hii inaashiria kifo cha Wanabutangi baada ya kukosa maji
pale kisimani.Hii ni baada ya kanuni mpya za utekaji maji kutolewa
amabazo ziliwanyima haki za kuteka maji. Maji ni uhai hivyo kupewa siku
tatu za kuteka maji ni kunyimwa uhai yaani kifo.
Jalada
Jalada ni karatasi ngumu inayofunika kitabu ambapo jina la kitabu
huandikwa.Katika tamthilia hii kuna picha ya mtu aliye na huzuni.Mtu
huyu ni kama ako katika shimo. Hii inaashiria shimo la mateso ambalo
Wanabutangi wametiwa na utawala mbaya wa Bokono na vibaraka wake.
Kuna picha inayoashiria machea.Hii inaonyesha matumaini kwa
Wanabutangi baada ya Mwelusi na wenzake kuanza harakati za
mabadiliko.Rangi inayotumika kwa picha ni ya udongo, kuashiria rotuba ya
Butangi.
DHAMIRA YA MWANDISHI
Kiini cha jambo au habari iliyoandikwa na mwandishi.Katika Kifo
Kisimani Kithaka wa Mberia ananuia kuamsha au kumchangamsha msomaji
kuhusu utawala mbaya na jinsi ya kuleta mabadiliko na kuuondoa .
Mwandishi anatetea haki za walionyanyaswa.Hivyo lengo kuu la mwandishi ni kuzindua watu.
PLOTI
Huwa ni mtiririko wa matukio katika kitabu.Tamthilia hii ina onyesho kumi.Muhtasari wa onyesho hizi ni kama ifuatavyo.
Onyesho la kwanza
Mchezo unaanza asubuhi ambapo viti vimepangwa tayari kwa mkutano wa
Bokono.Mwelusi ambaye ni kijan anaingia uwanjani.Mawazo yake
yanadhihirika kupitia kwa sauti tunayosikia .Yanamkejeli Bokono kwa
ubinafsi wake na kuwanyanyasa wanabutangi.
Kaloo anaingia uwanjani kwa kutayarisha ,anamwona Mwelusi na anadhani
ni mmoja wa waliohudhuria lakini Mwelusi anamwambia alikuwa anapita tu
ni mawazo yaliyomshika mguu.Kaloo anafurahi kwa kuwa Mwelusi anawaza juu
ya Butangi si kama vijana wengine wanavyo waza kuhusu anasa. Mwelusi
anakubaliana naye na kuongeza kuwa ni wakati wa vita. Kaloo hakubaliani
naye na anamuomba amfafanulie matamshi yake. Mwelusi anamwambia kuwa
atamueleza siku nyingine kwa kuwa hahudhurii mkutano na anaondoka.
Mwelusi Batu anaingia kuukagua uwanja, anafurahishwa na
viti.Anapoelezwa kuwa Mbutwe seremala aliyeunda viti anadai kulipwa Batu
anasema aje amwone na amdai malipo ya mbuzi wawili.
Wanawake ndio watakaocheza katika mkutanowa Bokono Mtemi wa
Butangi.Batu anasema kuwa mtemi akifurahi,wanawake watafurahi.Azena
anaingia uwanjani ili kumsaidia kaloo kwa matayarisho.
Batu anaapoondoka Atega anaingia akifuatwa na Mwelusi. Wanashukiwa
kuwa wapenzi kwa kuwa kila mara wanaonekana pamoja.Naye kama Mwelusi,
anawafahamisha hatohudhuria mkutano.Batu anaingia tena uwanjani na
kuamrisha watu waitwe.Gege anaingia uwanjani huku akiwa anapuliza ala ya
muziki. Batu anamwambia ni muziki wa kuvutia, yeye anasema kuwa
anausifia uongozi wa busara wa Butangi. Kaloo anamhakikishai kuwa yeye
na jamaa zake ni wazalendo kamili na hawatasita kuhudhuria mkutano.
Batu anawasaidia kujitayarisha jinsi watamsifia Bokono;Bokono Bokono milele!!
Baada ya muda kidogo wanagundua kuwa watu hawaji kwa mkutano.Kaloo
anaenda Mingamiwili na kurudi lakini hakuwapata watu huko pia.
Bokono anapofika anapata hakuna watu kwa uwanja anakasirika sana.
Vibaraka wake wanamuahidi kuwa kuna tatizo lakini watalinyoosha. Zigu
anasema kuwa watu wamechochewa na Mwelusi.Hata hivyo Batu anasema kuwa
watamkomesha anayewachochea watu.Baada ya mabo kutulia wote wanaanza
kumsifia Bokono ;Utaongoza Butangi kwa miaka mia moja.
Onyesho la pili
Matukio ni katika makazi ya Mtemi Bokono amabayo ni sehemu ya
majengo ya Utawala wa Butangi.Bokono amesimama huku akiangalia vitu
vilivyo ukutani na mara kwa mara anaguza hiki na kile.mkewe Nyalwe
amekaa kitini raha mustarehe, akjipepea.punde Mgezi anakuja hadi alipo
Nyalwe na kumuambia kuwa chakula kiko tayari.
Wanapokaa kula Bokono hali chakula ana wasiwasi sana. Nyalwe
anapomuuliza ni kwa nini hali anamjibu kwa kejeli na kumuuliza juu ya
vyeo vyake;mke, mwndani na msiri wake.
Nyalwe anamueleza Bokono kuhusu ndoto yake .Bokono anakubali kuwa ana
hofu ya kunyang’anywa utawala.Nyalwe anamuomba abadilishe mienendo yake
na anamuonya dhidi ya vibaraka wake wanoandanganya kuwa anapendwa na
Wanabutangi.
Bokono anapiga nduru kuwa amamwona nyoka ,anasema ameumwa na bafe
lakini wanagundua kuwa hamna nyoka mle ndani ni hofu tu ya Bokono.
Nyalwe anampa Bokono habari kuhusu kijiji cha Mama Agoro ambao
wangependa kuwagawia huzuni.Hii ni baada ya uwanja wao wa watoto
kuchezea umepewa Askari mkuu.Mama Agoro aliahidi kuridi tena na tena
kutetea haki yao.
Onyesho la tatu
Onyeshao hili ni katika gereza. Gereza ni chumba chenye kidirisha kimoja, kuta na sakafu chafu.
Tunaonyeshwa mateso na dhuluma kwa Mwelusi kutoka kwa Mweke na Talui.
Wanaanza kwa kumita mtukufu mtemi anaponyamaza wanazidi kunchapa na kumsukuma hapa na pale.
Mwelusi analalamika kuwa taya zake zinawaka moto kwani waliodai wamekuja kuzungumza naye wanafanya hivyo kwa mateke na makofi.
Wanamhoji Mwelusi na kumuuliza kama yeye ni mwelisi wa Biuki na kama
anatoka kijiji cha Bunyanya na ukoo wa langile.Anapojibu wanamsifu kuwa
yeye ni muungwana na ni kiongozi mzuri sana wa Butangi.
Wanamuuliza kama yeye ndiye kiongozi wa kundi la kabakaba.Wanazidi
kumchapa ili aliri kuwa anahusika na shughuli za ukombozi lakini
Mwelusi anakataa wanazidi kumachapa.
Batu anaingia na kuwakataza kumchapa, anaomba nafasi azungumze na Mwelusi.
Kwa upole anamshawishi Mwelusi akiri kuwa kiongozi wa wanamapinduzi na aombe msama kwa Mtemi Bokono.
Mwelusi anapolia juu ya maumivu Batu anamwambia kuwa atapewa dawa
nzuri akitoka gerezani baada ya kuomba msamaha.Batu anamuacha mwelusi
peke yake kwani anadai kuwa akili ya binadamu hufanya kazi vizuri akiwa
peke yake. Anaporudi na kupata welusi hajafanya uamuzi .
Antaka akiri kwamba anatumiwa na majirani ili kuchafua Butangi.
Anapotataa Btu anamwambia kuwa amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa
Askari na kuondoka.
Sura ya nne
Onyesho hili linatokea mbele ya gereza.Andua amemletea ndugu yake
chakula.Askari wanamkataza kumuona na Askari 111 anajaribu
kumdhurumu.Askari wanapanga kula chakula cha mfungwa lakini askari 1
anawakataza na kuwaomba wampe mfunwa chakula chake.anawaambia wenzake
kuwa ni walafi.wanazungumza kuhusu utawala wa mtemi Bokono kama utafikia
kilele au la.
Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache
kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza
kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi
hapo.badaye walimuua na kumzika msituni.
Onyesho la tano.
Onyesho hili ni nyumbani kwa Tanyauani.Tanya ameketi akidondoa nafaka
katika uteo.Kwenye sehemu nyingine ya ua Gege amekaakaribu na uzio
akiukaguakagua.punde anauachilia na kuanza kujishughulisha na
utengenezaji wa ala ya muziki.
Mamake anamuuliza kwa nini hajaenda kumtizama nduguye, Mwelusi kule
gerezani.Gege anwambia mamayake asimzomee.Anaendelea kutengeneza ala na
kusema kuwa wasichana watamtambua .
Katika kumbukumbu zake Mwelusi anarejea na kumuuliza hali ya uwnaja
wa ngoma. Wazungumza kuhusu hali ya wanabutangi.Gege anamshuritisha
nduguye kwa kujali jamii kila mara na kusahau maisha yake mwenyewe.
Mwelusi anamuomba aieonee huruma Butangi na awe mzalendao.
Andua anarejea nyumbani kutoka kisimani.Anajeraha upande mmoja wa uso
wake.Anamueleza mam yake kuwa hakupigana mbali amechapwa na Askari.
Azena anawatemebelea na kumtuliza Tanay juu ya mwanawe.Anamuomba asife moyo na azidi kumpelekea chakula.
Onyesho la sita
Onyesho hili ni nje ya gereza pia. Tanya amamletea Mwelusi chakula
na pia anataka kuonana naye.Askari wanchukua chakula na kuahidi kuwa
watampelekea. Tanya anapowaomba Askari kumwona mwanawe Askari 11 na 111
wanamkazata. Askari 1 anamuhurumia Tanya na kuwaomba wenzake wamkubalie
mama huyo kumwona mwanawe.
Baadaye Atega analeta chakula zaidi cha mfungwa pamoja na
tembo.Askari wanakula chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee rafiki
yake mkate wa wishwa.
Askari 1 anawahadithia juu ya Makea na ulevi wake.Muda huu wote Mwelusi amekuwa akikata minyororo kwa tupa.
Baadaye askari 111 napoenda kuchungulia anamwona na kumwita mwenzake
atazame pia.Muda kidogo wanasikia umati wa watu .askari wote wanapotea
Mwelusi anafunguliw gereza na kupotea.
Onyesho la saba
Matukio ya onyesho hili ni katika ukumbi wa utawala wa Butangi.Kuna
mkutano kati ya Bokono na vibaraka wake.Lengo la mkutano huu ni kupata
suluhu la Mwelusi na uchochezi wake.
Kame anasema wamuachilie lakini batu anasema hawawezi kumwachilia
mhuni.Maoni yake ni kuwa Mwelusi anafaa kuuliwa.Batu anasema kuwa
wawandanganye watu kuwa Mwelusi amkufa juu ya ugonjwa wa moyo au
aachiliwe kasha njiani apigwe pembe na nyati.Kame anpinga wazo la
kumwaga damu ya binadamu.
Askari 11 naingia na kuwaarifu kuwa Mwelusi amatoroka
gerezani.anapoomba msamaha Batu anamuonya kuwa lazima wamtafute Mwelusi
na waijaribu kutoroka kutoka Butangi.
Bokono anajiunga nao na anaposikia habari za kutoroka kwa Mwelusi
anakasirika na anawaomba wampe heshima yake. Baadaya anawaomba vibaraka
wake au wazee wamtafute na kumuua.
Batu anatumia Mweke na Talui kumshawishi Gege.Anamwambia amlete pale
na kumshawishi.Mweke na Talui wanafanya walivyo ambiwa na Kumwahidi Gege
ndoa na Alida baada ya kumuua Mwelusi.Wanajifanya wao ni wavuvi wawili
na kuhadithi juu ya ndoa ya Gege na Alida.
Onyesho la nane
Onyesho ni uani kwa Tanya.Tanya anajishughulisha na kazi za
nyumbani.Batu anaingia na kumsalimu.Baada yakuamkiana batu anamwambia
kuwa amakuja kwa ziara ya kirafiki. Sitiari ya kozi na njiwa inatolewa
na Tanya.Batu anaulizia kuhusu Mwelusi .Hii ndio sababu yake kuja kwa
Tanya.
Azena anaingia huku akitembea kwa shida.Anasema jinsi walivyovamiwa
na mali yao yote kuchomwa.Batu anasema kuwa ni majirani wao waliowavamia
lakini azena anasema kuwa ni uongo walivamiwa na wahini wa kulipwa na
kina Batu.
Tanya na Azena wanajikumbusha nyimbo walizomuimbia Bokono.
Mwelusi ana Atega wanatokea na kwa kutumia shingo Tanya anawaelekeza
watoroke.Baada ya Batu kutoweka Mwelusi anaeleza mama yake alivyookolewa
na umati.
Askari wanakuja kwa fujo lakini Mwelusi na Atega wanfaulu kutoroka.
Kame anakuja pia na kufikia sasa Tanya anamkejeli kuwa utawala wa
Butangi umemtembelea imebaki Bokono Mwenyewe.Kame anawaeleza kuwa nyoyo
zao ziko pamoja nay eye ni mmoja wa wanamapindizi.Wote wanaondoka
kuelekea kisima cha mkomani aliko Andua na wanamapinduzi wengine.
Onyesho la tisa
Matukio ya onyesho hili ni kisima cha Mkomani.Ni asubuhi na zigu
amesimama huku macho yake yakilikagua bonde.Kaloo anatokea na anapofika
karibu na zigu zigu anashtuka.zigu anamuulizia kaloo kuhusu maoni ya
wanakijiji wnzake juu ya kannuni mpya zilizotangazwa.Anasema kuwa
kanuni zote za Butangi ni za busara.
Kaloo anamtuma zigu amshukuru Bokono Kaloo anamtuma zigu
amshukuruBokono kwa ajili ya kazi aliyoamuru mototo wake apewe.kaloo
hajali juu ya Butangi yeye anataka awe na uhusiano na Bokono ili apate
mali zaidi.Kaloo anaambiwa kuwa ni vyema aende akamshukuru mwenyewe
kwani hivi karibuni Bokona amekuwa akimtaja mara kwa mara.
Andua anapokuta kuteka maji zigu anamkataza na kumueleza kuhusu
kanuni.baadaye Mwelusi na Atega wanatokea lakini Zigu
hawatambui.Anawazungumzia kuhusu Mwelusi aliye gerezani.Zigu ako tayari
kutetea kanuni za Butangi hata kwa silaha.
Baadaye Gege anakuja na kumdanganya Mwelusi kuwa ametumwa na mama yao
Tanya huku akilia , ni ujumbe muhimu ambazo babayao alimwachia.
Wanaenda chemba na Gege anamuua.Kame anafika amechelewa na wote
wankimbia chemba baada kusikia sauti yenye huzuni.
Onyesho la kumi
Matukio ya onyesho hili ni katika Ukumbi wa Utawala wa Butangi.Kiti
cha mtemi kiko mahali pake,lakini ni kitupu.Batu ymo ukumbini.Punde
Mweke anaingia na baadaye Gege. Wakati Gege anadai malipo yake Baada ya
kumuua Mwelusi ndio anagundua kuwa alidanganywa.Batu anamwahidi kuwa
atapata zawadi ya ardhi.Bokono anapoingia anamwahidi kuwa atapewa jina
Mkuki wa Almasi.
Nyalwe anaingia kwa wasiwasi na kuwaonya kuwa umati wa watu
unakuja.wanampuuza.Hata hivyo wanashangaa kuwa Mweke hajaleta habari
zozote na Zigu pia hakuweko.
Azena anaingia ukumbini kama ameinua panga.Kisha askari1,Kame na
Atega.Atega anamtetea nyalwe asifungwe kwani alikuwa kamwe anatetea
Wanabutangi.Wanawafunga Bokono, Batu,Gege na kuwatoa nje .Watu
wanasherekea ukombozi wao.
WAHUSIKA
Wahusika ni binadamu wa kawaida na wanaendeleza shughuli za kawaida za kila siku za binadamu.
Mhusika mkuu ni
Mwelusi .Ni kiongozi katika shughuli za ukombozi wa butangi.Anafungwa katika jela na kuteswa sana.(uk 21) onyesho la tatu.
Gege ni nduguye Mwelusi yeye anaendleza maudhui ya ubinafsi.Hana utu,ni msaliti na pia muuaji kwani alimmuua Mwelusi pale kisimani.
Bokono ni kiongozi mbaya mwenye udikteta.Ananyanyasa na kukandamiza Wanabutangi.Anawanyima wanabutangi haki zao Kupitia vibara wake
Batu na Zigu.Viongozi hawa ni wakatili,hawana utu. Wanamdanganya Bokono kwamba anapendwa lakini huo ni unafiki wao.
Tanya na Azena ni wanawake wanao tetea haki za
wanabutangi.Tanya ni Mamake mwelusi na nimkakamavu anazozana na Batu na
habadilish msimamo wake.Uk 76 onyesho la nane.
Atega na Andua ni wasichana ambao wanashiriki
katika ukombozi ni wakamavu, wana ujasiri na pia ni wenye nidhamu hasa
Atega kwa kuwapa askari tembo na kumpelekea Mwelusi tupa.Hawa ni
wahusika wasaidizi.
Kuna wahusika wengi kama vile
Askari 11 na 111ambao wanaendeleza maudhui ya ukatili na dhuluma pamoja na
Mweke na Talui.
Kame na
Askari 1 ni wenye utu na wamezinduka na kushiriki katika ukombozi.
Kaloo ni kibaraka wa Mtemi Bokono.Yeye hajazinduka.Ni mwenye ubinafsi na anamtetea mwanawe.Ni mfisadi
MANTHARI
Ni mahali au mazingira yanayotumika katika kitabu. Mazingira ya
kawaida yametumika katika tamthilia hii.Kuna mazingira ya kinyumbani
kama vile Kwa Tanya, Nyumbani kwa Bokono uk 12 onyesho la pili.Kuna
mazingira ya uwanjani, kisimani na gereza.
MBINU ZA UANDISHI NA ZA LUGHA
Kejeli uk 21 Mweke na Talui wanawita Mwelusi Mtukufu
Mtemi.Hii ni kejeli kwani Mwelusi si mtemi mbali ni kiongozi wa
ukombozi.Kejeli inasaidia kuendeleza maudhui ya dhuluma.
Matumizi ya
Ndoto uk 14 Nyalwe mkewe Bokono
antuhadithia jinsi usiku mmewe alikuwa akiota na kusema watu wamtoe
kaburini. Ndoto hii inaonyesha hofu ya Bokono kutokana na utawa wake
ambao ni mbaya.Ndoto hii inaendeleza maudhui ya Hofu na utamaushi.
Kuna
Nyimbo uk 81Azena na Tanya wanakumbuka nyimbo
za kumsifia Bokono. Wimbo huu unaonyesha Bokono kama kiongozi bora asiye
na kasoro.Wanabutangi waliimuinua Bokono karibu na mungu.Maudhui yake
ni ya uongozi wa kidkteta.
Kuna matumizi ya
Taswira.Hizi ni picha zinazojengeka
katika akili ya msomaji.Mwandishi ametumia taswira mbalimbali kama vile
gereza.Uk 21 gereza imechorwa kama mahali penye kidirisha kimoja ,kuta
na sakafu chafu. Picha hii inasaidia kuendeleza maudhui ya dhuluma na
kunyimwa haki kwa mfungwa.
Takriri imetumika uk 6 ambapo Kaloo, Azena na Gege
wanakariri Bokono Bokono Milele mara kadhaa.Hii inasaidia kumpa Bokono
matumaini ya kuwa anapendwa.Huu ni Unafiki.Kuna takrir pia katika kurasa
zifuatazo uk 8,11,14
Tashhisi imetumika katika ukurasa wa kwanza ambapo
sauti inasema kuwa jua lina bahati,jua lina uwezo uwezo mkubwa. Mwelusi
pia anasema mawazo yamemshika miguu kuonyesha hofu aliyonayo.askari
wanasema kuwa siku inajikokota. Uk 53.Hii inaonyesa ukatili wao na
dhuluma na mateso wanayomletea mwelusi. Andua anaambiwa na Askari
asipoondoka atatemebelewa na makofi.Hii ni dhuluma.
Tashbihi ni ulinganisho wa moja kwa moja wa vitu au
watu na wanyama. Mfano uk71Alida bintiye mtemi ana shingo ya upanga.Hii
ni kusaidia kumshawishi Gege na maelezo haya yanaendeleza unafiki kwani
ndoa anayoahidiwa na hurulaini haipo. Uk 37 Askari wanasema uharibifu wa
mwelusi uko wazi kama meno ya ngiri.
Jazanda ni picha inayomwingia mtu akilini na
kuilinganisha na hali ya kawaida.Mfano uk 61 Batu anaashiriwa kama macho
na masikio ya Butangi, uk64 mwelusi ni mwiba wa Butangi.Hii ni tofauti
na jukumu lake la kuleta mabadiliko katika utawala wa Butangi lakini si
kuzuuia maendeleo.
Methali mfano uk55 Batu anasema kuwa dawa ya moto ni
moto. Hii ni katika hatua aliyochukua ya kutumia watu kuvamia kina
Azena.Huu ni ukatili wa kiwango cha juu. Methali pia zimetumika katika
kurasa zifuatazo 16,52,39,102 na kadhalika
Chuku ni kutia chumvi au kuongeza sifa ili jambo au
kitu kiwe cha kuvutia. Mfano uk 71 Maelezo ya Alida yametiwa chumvi ili
kumvutia Gege.
Katika uk 9 baada ya mambo kutulia na hasira ya mtemi Bokono Kuisha
Batu,Zigu,Kaloo, Azena na wengine waliofika wanaanza kumsifia Bokono
;Utaongoza Butangi kwa miaka mia moja.Hii ni chuku kwani Mtemi
ameshazeeka na hawezi kutawala kwa miaka mia moja.
Chuku pia imetumika katika kurasa zifuatazo 30,72,56 na kadhalika.
Semi uk27 Mwelusi anasema koo lake liko motoni.Hii
ni baada ya kichapo na mateso anayopata gerezani.Semi hii imetumika
kuonyesha dhuluma na mateso kwa Mwelusi. Askari 11 anaeleza jinsi
walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe
binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza kuwa popo na
baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi hapo.Inamaanisha
kuwa walimvuta na kumkata na kumdhulumu sehemu zake za siri.
Semi pia zimetumika katika kurasa zifuatazo 15.27,37 na kadhalika
Mwandishi ametumia
Lugha ya Matusi. Hasa katika mazungumzo ya Bokono na Nyalwe.Mfano mwehu
MAUDHUI
Mambo muhimu yanayoelezwa katika tamthilia.Mwandishi ameshighulikia
maudhu kuu kama vile uongozi mbaya, dhuluma na mateso,ubinafsi na
ukombozi.maudhui mengine ni kama vile usaliti, ubinafsi, utu, unafiki na
uchochezi.
Uongozi Mbaya
Mtemi wa Butangi Bokono pamoja na vibaraka wake Batu na Zigu
wanaendeleza maudhui ya uongozi mbaya. Wanamfanya Mwelusi kukamatwa na
kufungwa gerezani bila makosa yoyote amabayo wanaweza kuthibitisha.
Katika Mkutano batu anaeleza jinsi walichoma kijiji cha Kina Azena na kusema mfumo wake wa uongoni ni dawa ya moto ni moto.
Kwa kuwa Mwelusi anatetea haki za wanyonge Bokono anamwita mwiba. Hii
ni kwa sababu anazuia yeye na vibaraka wake kujichumia mali. Mwishowe
wanamtumia Gege kumuua.
Wanaamua kuwanyima Wanabutangi haki ya kuteka maji pale kisimani.
Mtemi anauliza kamawamewatangazia watu kuhusu kanuni mpya ya kuteka maji
kisima cha Mkuyuni kuwa ni siku tatu kwa wiki.
Dhuluma Na Mateso
Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache
kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza
kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi
hapo.badaye walimuua na kumzika msituni.uk 43
Mwelusi anafungwa gerezani kama hakuna kesi na hajahukumiwa.Batu
anapomtemebela baada ya kumshawishi akiri kutochochea Wanabutangi na
kushindwa anawaagiza Askari wazidi kumchapa na kumtesa.uk 29
Katika uk 30 Mwelusi anasema anachomwa na mikuki mia moja na
anaelezwa kama anayeumia.Hii ni kutokana na kichapo anachopata kutoka
kwa Askari.
Uk49 Andua anasema kuwa hakupigana alipigwa na ndia sababu ako na
jeraha upande mmoja wa uso wake.Anasema kuwa ni Ni Askari waliwapiga
kule kisima cha Mkuyuni baada ya wao kwenda kuteka maji.
Askari wa Butangi kulingana na Tanya si wa kulinda mbali ni wa kuleta
mateso na kuwachapa Wana butnagi. Tanya anasema kuwa juzi walimngoa
motto wa Chendeke meno.
Uk 24 Mweke na Talui wanapokuja kuzungumza na Mwelusi wanafanya hivyo
kwa makofi na mateka.Mwelusi anasema kuwa taya zake zinawaka moto.
Batu anajaribu kuukinga uongozi wa Bokono na amamuomba mwelusi kuacha
uchochezi na kuomba msamaha.Mwelusi anapokataa kukiri kwamba anatumiwa
na majirani ili kuchafua Butangi. Anapotataa Batu anamwambia kuwa
amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa Askari na kuondoka. Yeye anawpa
ruhusa Askari wamtese mwelusi badala ya kumlinda.uk 36
Ubinafsi
Tunauona ubinafsi wa Gege .Uk wa 95 Gege anamuua Mwelusi nduguye ili
apate kuozwa Alida bintiye Mtemi. Uk 17 anamuambia Mwelusi ajali maisha
yake aachane na jamii. Gege hajali maisha ya wnabutangi wengine
anajijali yeye mwenyewe.
Uk 89 Kaloo anamtuma zigu kwa Bokono amshukuru kwa ajili ya kazi
aliyoamuru mototo wake apewe.kaloo pia hajali juu ya Butangi yeye
anataka awe na uhusiano na Bokono ili apate mali zaidi.
Gege hajaenda kumtizama nduguye, Mwelusi kule gerezani.Gege anwambia
mamayake asimzomee anapoulizwa.Anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa
wasichana watamtambua .Hivyo anajali sana wasichana kuliko nduguye.uk43
Ukombozi
Mwelusi,Atega.Andua,Kame na Askari 1 ni baadhi ya wanamapinduzi katka Butangi.
Watu hawa wanapinga utawala wa Mtemi Bokono na vibaraka wake.
Wakati Mwelusi amefungwa gerezani Atega anamletea mkate wa wishwa
ukiwa na tupa ambayo anatumia kukata minyororo na kujikomboa. Baadaye
umati wa watu wanakuja na kumsaidia kufungua gereza na kujikomboa.uk 59
Kwa Uongozi wa Mwelusi wanaendelea kutetea haki zao.Mfano Andua anaenda kisimani kuteka maji.
Hata baada ya mwelusi kuuliwa na Gege wanamapinduzi hawa wanaendelea na harakati zao za ukombozi. Uk 105
Kitabu kinaisha kama Bokono,Batu,Zigu , Mweke na Gege wamefungwa
kamba baada ya kufumaniwa na Waandamanaji.Hivyo wanaukombozi wanafaulu
kukomboa Butangi kutokana na utawala Mbaya.
Mwelusi anadaiwa kuwa yeye ndiye kiongozi wa kundi la kabakaba.
Anahusika na shughuli za ukombozi.Ni yeye kiongozi wa kundi hili la
wanamapinduzi.
Usaliti
Gege anamsaliti kakake, Mwelusi kwa Kumuua pale Kisimani. Uk 95 Gege
anamdanganya Mwelusi kuwa ametumwa na mama yao Tanya huku akilia , ni
ujumbe muhimu ambazo babayao alimwachia. Wanaenda chemba na Gege
anamuua.
Viongozi wa Butangi ikiwemo Batu na Zigu wanawasaliti kwa kuwanyima haki zao na kuwatesa.
Utu
Kame Askari 1 ni wenye utu wanamtetea Mwelusi.
Uk 60 wakati Batu na zigu wanataka kumuua Mwelusi Kama anasema wamuachiliea kwa kuwa hana makosa yoyote.
Uk 35 Tanya anapowaomba Askari kumwona mwanawe Askari 11 na 111
wanamkazata. Askari 1 anamuhurumia Tanya na kuwaomba wenzake wamkubalie
mama huyo kumwona mwanawe.
Hawa wawili paoja na wengine kama vile Azena na Atega ni wenye utu
miongoni mwa wanabutangi wengi ambao wana unyama kama vile Batu.
Askari wanapanga kula chakula cha mfungwa lakini Askari 1 anawakataza na kuwaomba wampe mfunwa chakula chake.uk 37
Unafiki
Uk 25 Mweke na Talui wanamhadithia Gege jinsi harusi yake na Alida
itakavyokuwa. Wanamwambia Gege amuue Nduguye Mwelusi na atapewa mali
pamoja na kuoa mtotot wa Mtemi Bokono.
Wakati Gege anaenda kudai malipo yake Baada ya kumuua Mwelusi ndio
anagundua kuwa alidanganywa.Talui na Mweke ni wanafiki walijua kuwa
wanamdanganya Gege ili awasidie tu kumumaliza Mwelusi.
Batu anapomtemebelea Mwelusi gerezani anamwambi a kuwa ni rafiki yake
na kumuomba ajiunge naye katika kuitumikia Butnangi.Huu ni unafiki
kwani kabla ya hapo alipokuwa kwenye mkutano na Zigu na Kame alpanga
jinsi watakavyo muua.
Uk 79 Batu anapomtembelea Tanya anamwita rafiki yake tangu ujana wao.huu ni unafiki kwani Batu yuko pale kumtafuta Mwelusi.
Baada ya kumuahidi Tanya kuwa watampa Mwelusi chakula Askari wanakula
chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee rafiki yake mkate wa
wishwa. Uk 58. Huu ni unafiki.
Uchochezi
Kabla mkutano uanze Mwelusi anafika pale na kudai kuwa anapita.Hata
hivyo nia yake wakiwa na Atega ni kuwachochea watu wasuhudhurie mkutano
wa Mtemi Bokono.Uk 1
Uk wa 9 Zigu anasema kuwa kuna fununu ya kuwa kuna kijana anayechochea watu.Kijana huyu ni Mwelusi.
Uk 90 Zigu anamwambia Kaloo kwamba Bokono amekuwa akimtaja mara kwa
mara.Zigu ananchochea Kaloo aonane na Bokono na kumpa shukrani yeye
mwenye kwa kazi ambayo Bokono alamuru motto wa Kaloo apewe.
FALSAFA YA MWANDISHI
Mwandishi analenga kuzindua wananchi kuhusu utawala mbaya.Anatetea
haki za walionyanyaswa na kukandamizwa. Anashikila kuwa kuna uwezo wa
kujikomboa kutoka kwa uongozi mbaya .Hii ni kupitia kwa watu kuungana na
kuandama na kutetea haki zao na kubadilisha uongozi mbaya ,pamoja na
kuwafungaviongozi wabaya.
Falsafa ya Kithaka ni haki na hukumu kwa wenye makosa.
NADHARIA
Mwandishi ametumia Nadharia kama vile
Umaksi.Katika Butangi wenye mali wananyanyasa wasio na mali.Kuna
Ufeministi kwani Atega ,Andua Tanya na Azena ni wahusika wa kike wanaoshiriki katika ukombozi.Kuna
Uhalisia Kwani matukio ni ya kawaida kam vile uongozi mbaya na kunyimwa haki katika maisha ya kila siku. Kuna
Utamaushi kwani wanabutangi wamekata tama.Mfano Tanya anamtaka Mwelusi aondoke Butangi
HITIMISHO
Mwandishi amefaulu kutumia mbinu na kutoa maudhui kwa kutumia
nadharia. Kithaka anatetea haki kwa wenye Kunyanyaswa na hukumu kwa
wenye makosa.Amewatumia wahusika wa kawaida kuutoa ujumbe wake.
Kuna udhaifu katika anwani kwani sio wahusika wote wanaathiriwa na kifo kisimani.Kitabu kimeshughulikia zaidi ya kifo.
UHUSIANO KATI YA TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI NA UTENZI W A FUMO LIYONGO
Utenzi wa fumo liyongo unamhusu shujaa Liyongo kutoka jamii ya
waswahili.liyongo alishuhudiwa na jamii yake na makabila jirani kama
vile wagalla.
Hata hivyo mfalme wa pate(Daudi Mringwari) alimchukia kwa kuhofu kuwa
angemnyang’anya utawa wake.Hivyo alipanga njama za kumwangamiza
liyong.Akamtia gerezani alikolindwa na Askari wake.Akiwa gerezani,
aliletewa mkate wa wishwa uliotiwa tupa.Aliitumia tupa hii kukata
minyororo kasha akotoroka.
Mfalme wa pate hakukata tama.Alimshawishi mwanawe Liyongo kumuua
babake na kumwahidi kumwoza bintiye.Liyongo akauliwa na mwanawe kwa
kumfuma msumari wa shaba kitovuni.Liyongo alifia kisimani na kuwatisha
watu wasichote maji kwa siku kadhaa.
Utenzi huu kwa kiasi kikubwa unahusiana na tamthilia ya Kifo
Kisimani, inayomhusu Mwelusi anayepinga utawala dhalimu wa Mtemi Bokono.
Anachukiwa na Bokono pamoja na vibaraka wake kwa hofu kuwa atauangusha
utawala huo.Anatiwa gerezani lakini anatoroka baada ya kukata minyororo
kwa tupa iliyotiwa ndani ya mkate wa wishwa alioletewa na Atega. Bokono
anamtumia nduguye Mwelusi, Gege kumuua kwa kumdunga kisu pale kisimani.
Gege vilevile anaahidiwa na Mweke wakiwa na Talui kuwa ataozwa bintiye
mtemi.Alida.
Hata hivyo kuna tofauti nyingi kati ya tungo hizi mbili. Fumo Liyongo
ni mhusika wa kihistoria, aliishi baina ya karne 15 na 16.Mwelusi naye
ni mhusika wa kubuni.Fumo alikuwa na sifa za kiajabu kama vile nguvu
zilizokithiri, mpiganaji hodari aliyeshinda vita vingi, ukubwa uliopita
kiasi na uwezo wa kutambua mabo kabla hayajiri.Mwelusi hana sifa kaa
hizi zinazomtambuliasha kama mhusika wa kipekee.Vita anavyopigana si vya
silaha bali anapinga dhuluma na mateso kwa Wanabutangi.
MAREJELEO.
- Kithaka wa Mberia, (2001) Kifo Kisimani, Marimba Publications limited, Nairobi Kenya.
- Rocha M.Chimera, (1998) Kiswahili; Past, Present and Future Horizons,Nairobi University Press,.Nairobi.