Search This Blog

Tuesday, 28 April 2015

Mwongozo wa Riwaya ya Mwisho wa Kosa, Mwisho wa Kosa,

Mwongozo wa Riwaya ya Mwisho wa Kosa

25 Apr
CHUO KIKUU CHA EGERTON
JINA :Jacqueline Kamau
NAMBARI YA USAJILI: A13/30196/08
KITIVO: Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
IDARA:Fasihi ,Lugha na Isimu
KODI YA KOZI: KISW 411
KOZI: Fasihi linganishi
KAZI:Uchambuzi wa riwaya ya Mwisho wa Kosa
IMEWASILISHWA KWA:Bw.Gacheiya
TAREHE: 04/04/ 2012





RIWAYA YA MWISHO WA KOSA
Utangulizi
Riwaya ya Mwisho wa kosa imeandikwa na Z. Burhani.Ilichapishwa mwaka wa 1987 na Longhorn Publishers (k) Ltd.
Anwani
Anwani huwa ni jina la kitabu. Mwandishi amefaulu kutumia anwani’Mwisho wa kosa ’. Anwani hii inaashiria Mwisho wa Makosa ya Monika hasa kwa wazazi wake. Pia anwani hii inaashiria  mwisho wa kosa la Ali na jinsi anavyopata kazi hata baada ya kufukuzwa chuoni.Pia ni Mwisho wa Kosa la Rashid la kuishi na Monika na pia ufisadi wake.
Jalada
Jalada ni karatasi ngumu inayofunika kitabu ambapo jina la kitabu huandikwa.Katika riwaya hii kuna picha ya watu wengi.Kuna wenye suti ambao huenda ni mawaziri Matata na Selemani au Rashid. Kuna picha ya ndege kuashiria ndege ambayo Monika alisafiri nayo kwenda ng’ambo.Pia kuna picha ya seremara. Kuna pesa ambazo zinapewa mkono wa mtu kuashiria ufisadi wa Rashid na wengine.Kuna picha ya nyumba za kijiji huenda ni pale kijijini kwa kina Monika.
Dhamira ya mwandishi
Dhamira ni kiini cha jambo au habari iliyoandikwa na mwandishi.Katika Riwaya hii mwandishi ananuia kutuonyesha athari za masomo ya ulaya na kwingineko.Amemtumia Monika kuonyesha jinsi elimu inavyombadilisha mtu.
Hivyo lengo kuu la mwandishi ni kuonyesha kukengeuka .
Manthari
Ni mahali au mazingira yanayotumika katika kitabu. Mazingira ya kawaida yametumika katika riwaya hii.Kuna mazingira ya kinyumbani kama vile nyumbani kwa Mhaji na Nyumbani kwa Selele uk 12.Kuna mazingira ya  uwanja wa ndege,ofisi na kadhalika.
                                                                                        
PLOTI
Huwa ni mtiririko wa matukio katika kitabu.Riwaya hii ina sura Kumi. Maelezo ya sura hizo ni kama ifuatavyo.
Sura 1
Monika anarejea kutoka ulaya alikokwenda kusoma. Waliokwenda kumlaki wanaonyeshwa dharau pale uwanja wa ndege.Tunaelezwa kuhusu kesi ya Asha na Bi keti  amabapo katika Uk 29 Keti anakamatwa na polisi na kesi yao kuanza.
Monika wanazozana na keti kuhusu uji.
Sura 2
Tunaelezwa mpango wa wazazi wa Ali juu ya ndoa ya Ali na Zabara uk 54.Tunaelezwa jinsi ndugu na dadake zake Ali wanavyosumbuliwa na wasichana pale kijijini.
 Sura ya 3
Monika na Muna wanakutana.Hawa ni wasichana wawili ambao wamesoma.Uk 55  kuna mazungumzo kati ya monika na Muna ambapo Monika anamuuliza Muna maswali juu ya ndoa yake.
Ugomvi baina ya Monika na Babake. Na Monika anaondoka kwao.Pia kuna ugomvi kati ya  Rashid na Monika wanapoishi pamoja.
Sura ya 4
Katika hii sura maudhui ya ufisadi yanajitokeza. Ufisadi kati ya Rashid na Alison.Ambapo Alison anapata kandarasi .Pia Mheshimiwa anataka kumhonga Rashid ili apate kandarasi pia.Tunaelezwa Kazi ya Rashid katika ofisi yake.
Sura ya 5
Monika anakutana na Mheshimiwa Selemani na kuuelewa unafiki wa Juma.
Tunaelezwa jinsi masomo ya Ali na jinsi madawaya kulevya yalimfanya afukuzwe shule.Uk 121 kuna barua ya kufukuzwa kwa Ali kutoka chuo kikuu.
Sura ya 6
Rashid anaenda kwa Saidi kupata ushauri,anahisi kuwa alikosea kwa kushiriki  ufisadi.Mhaji anamtemebelea Selele  na kumuomba amzungumzie Monika na amsaidie Monika kama mwanawe.Mhaji anataka monika aunganishwe na familia yake.
Sura ya 7
Karne anamsaidia Ali katika kazi yake mpya. Karne anaeleza kosa la shilingi 17,000 badala ya shilingi 1700.Hii ni hadithi ndani ya riwaya.
Kuna maelezo juu ya ugomvi wa Muna na Hasani katika ndoa yao mabayo in matatizo mengi mno.
Sura ya 8
Ali anapata kazi mpya ofisini kwa Alison. Waziri Salimu anashindikizwa kumfuta kazi Rashid.Baadaye  Rashid anapata kazi katika kampuni ya Alison.
Uk 199 Monika anahama kwa Rashid  na kwenda kwa nyumba mypa aliyopewa ma Matata. Kuna ugomvi kati ya Matata na selemani kuhusu Monika.
Sura ya 9
Ndoa ya Hasani na Muna ambayo imejaa ugomvi inavunjika na Muna kurudi kwao.
Sura ya 10
Matata namuacha Monika na Kuoa msichana mwingine.Monika anarejea kwao na kuolewa na Shabani.Ali na Sara wanapata kujuana na Kupanga kuoana. Riwaya inakamilka kwa sherehe nyumbani kwa Selele.Rashid anakuja na Salama,Monika na Shabani, Muna na Hasani.







WAHUSIKA
Wahusika ni viumbe walio katika kitabu.Katika Mwisho wa Kosa wahusika ni binadamu wa kawaida na wanaendeleza shughuli za kawaida za kila siku za binadamu.Riwaya hii ina Wahusika wengi kama vile.Ali,Saidi na Selemani.

Mhusika mkuu ni Monika .Ni Mjeuri uk 13 keti anajilaumu kwa kumpiga monika ,alielewa kuwa kwa desturi maneno na jeuri ya Monika yasingemshughulisha. Ni mwenye dharau hasa kwa Keti. Amekengeuka na ni mwenye tamaa ya mali kwani anafuatana na wanaume ili apate pesa na abebwe  kwa magari ya kifahari. Alisoma  huko ulaya.
Uk 89 ni mpenda anasa tokea siku ile Monika alipokutana na Juma, alikuwa kila siku yuko safarini.

Asha  ni mwenye wivu na Mgomvi.Uk 26 anamfanya Keti akamatwe na polisi.Anasema uongo kuhusu Keti.
Muna ni mpole, mvumilivi,mwenye heshima na mwenye bidii.Aawaheshimu wazazi wake na mumewe. Ana uhuru na amejikomboa kutoka kwa utamaduni.Uk 243 tunaelezwa jinsi alivyotoka kwa mumewe baada ya kugombana naye. Anapenda kusoma.

Rashid ni msomi,Mfisadi.Ameshindwa kumfukuza Monika kwake.Ana heshima kwa wazee kama vile Selele na Keti ambao wanamshauri.
Salama ni mpole na rafiki ya Monika.Anaposwa na Rashid na mwishowe wanaoana. Ni mvumilivu kwani alimsubiri Rashid kwa muda mrefu baada ya posa lake.

Hasani ni mkatili hamsaidi bibi yake,anamkataza kutoka na kumgombeza.Ni mchoyo na mwenye wivu.Hana utu na ni mgomvi sana.
Matata ni mnafiki anamdanganya Monika kuwa atamuoa lakini mwishowe anamtoroka.Anamwonea Rashid wivu na kufanya afutwe kazi.
Alison ni mfisadi na mwenye utu.Anawaajiri Ali na Rashid.
Selele  ni mzee mwenye nasaha.Anaunganisha familia ya Mhaji.Ni mkarimu na mwenya utu.
Mhaji ni mlezi bora anampenda mwanawe.Una utu na anashirikiana na jamii.

MBINU ZA UANDISHI NA ZA LUGHA
Kejeli uk 12 Bi Keti anamwita Monika bi mzungu” Naye bi mzungu huko ulaya aloko kwanda….Kejeli hii inaendeleza maudhui ya ukenegeuko na ujeuri .
Uk 252 Monika anawaambia wafanya kazi , watamuona atakapokuwa mke wa waziri…ndio mke wa waziri .wanamcheka baadaye mwenzake anamwambia  kuwaMwajiri wao Mheshimiwa Matata anapanga Harusi na msichana mwingine.
Matumizi ya Ndoto uk 82 Rasid aliota kwamba yoko Mahakamani kama ameshatakiwa kwa kosa la uhaini na yeye akijaribu kujitetea kwa nguvu zake zote….Ndoto hii inatuonyesha wasiwasi kwa Rashid. Ndoto hii inaonyesha hofu ya Rashid.
 Barua
uk 118 Barua ya kufukuzwa shule kwa Ali.Mzee Bushiri anaelezwa ni kwa nini mwanawe amefukuzwa shule.uk 215 barua ya Ali kutoka ka J.R Alison ya kumpa kazi.Ali anapata kati katika kampuni ya AlisonUk 227 Salama anamtumia Barua Rashid na kumueleza juu ya ndoa yao.Salama anamwondolea Rashid jukumu la posa iliyotolewa na wazazi wao wangali wadogo.Anamwambia si lazima wafuate hayo.
Dialojia Riwaya hii imetawaliwa na dayalojia mabayo inasaidia kuendeleza ploti.Ni kupitia mazungumzo baina ya wahusika tunapa kuenedeleza maudhui ya unafiki ,ufisadi na malezi mema.
Taswira. Uk 10 tunapa picha ya mahali Amina nduguye monika aliendea uji.Pia kuna taswira ya jinsi Monika na keti wanavyopigana.
Kuchanganya ndimi.Uk 60 maneno ya kizungu yanatumika Msimbiji Street na Zambia avenue.Uk 176 kuna matumizi ya jina metropolitan
Sadfa  uk 102 Wakati wa mapumziko Monika altembea kwenda madukani kununua viatu.Alikuwa amechoka na alitama Juma angembeba kwa gari lake. Monika alijifuta jasho usoni na kisadfa Monika aliliona gari la juma kwa upande Mwingine.
Methali uk182 Selele  anawaeleza wageni wake kuhusu suala la masomo na ustaarabu. Akili huja kwa maarifa.Methali zingine ziko katika kurasa zifuatazo.13,na 126.

Tashbihi ni ulinganisho wa moja kwa moja wa vitu au watu na wanyama. Mfano uk 34 Monika amekuwa kama sahani ya santuri ambayo imekwarizika.Hayaelewi maisha yake.amekengeuka sana. Tashbihi zingine ziko katika kurasa zifuatazo.112 na 26.
Semi Muna anamwona minika kama asiye na uwezo wa  kuona mbele wala nyuma.Akili yake imepoteza mizani na kusahau thamani ya yale yake na kutaka kutabaka yaw engine.Uk 34
Utohozi Uk 120 baba ya Ali alikuwaakisikiliza redio.(radio)Hili ni jina la kiingereza ambalo limeswahiliswa,utohozi mwingine unapatikana uk179 na 52.
Tashhisi uk111 Akili ya ali inapewa uwezo wa kuchoka,kupumzika,kujikusanyia nishati na kuweza kuendelea na kazi zake.Tashhisi zingine zinapatikana katika kurasa zifuatazo, 13, 105, 118, 164 na 203
MAUDHUI
Mambo muhimu yanayoelezwa katika tamthilia.Katika riway hii mauthui muhimu ni yaUkengeuko.katika ukengeuko kuna maswala kama vile utamaduni,elimu, malezi na mahusiano ya kijamii.Maudhui haya yanaweza kuelezwa kama ifuatavyo;

Mkengeuko
Wakati Monika anaporejea kutoka ulaya anakataa kuwajulia hali waliokuja Kumpokea  pale uwanja wa ndege.Hii si kawaida kwani watu hao walimsherekea kwa nyimbo lakini yeye anaonyesha dharau kwao.

Uk10 Monika anasema kuwa uji wa bi keti na samaki wa kukaanga ni chakula kichafu na kinaweza kusababisha magonjwa.Kulingana na Bi Keti ni ji huu ndio uliomlea yeye.Hivyo mbona hukumletea magonjwa wakati alipokuwa akiunywa
Uk 60 Monika anahama kwao na kwenda mjini kuishi na Rashid.Hii si kawaida katika utamaduni wao.Msichana anafaa kuhama kwao akienda kwa mume wake.

Uk 58  Monika anamwona Salama kama mjinga,Hakusoma na si mrembo hii ni athari ya ulaya kwani kabla ya monika kwenda Ulaya walikuwa marafiki wa dhati na salama.
Uk 76 Monika anakwenda dansi na kuridei saa tisa kasorobo usiku.

Utamaduni
Utamaduni ni mila,asili, jadi na desturi za kundi la jamii Fulani.
Mfano katika jamii ya Mwisho wa Kosa kuna tamaduni ya kupeleka posa kwa wazazi wa msichana kutoka kwa wazazi wa mvulana.Kuna pia harusi ambazo zinafuata tamaduni.

Mhusika Monika anakiuka tamaduni sana. Mfano Uk 60 Monika anahama kwao na kwenda mjini kuishi na Rashid.Hii si kawaida ya wasichana,kwani mtu anafaa kutoka kwao akienda kuishi na mume wake.

Ndoa ya Muna na Hasani ni mfano mwema wa ndoa za kitamaduni. Hata hivyo Muna anajikomboa na tamaduni hizi, kiasi cha kwamba Hasani analalamika kuwa Muna hamtumikii mumewe.Mamake Muna anamshauri jinsi ya kumtunza mume na kumfurahisha.Hata hivyo Muna anafuata usasa na kushiriki mambo amabayo yametengewa wanaume na utamaduni ama vile siasa.

Katika ukurasa wa 76 Monika anakwenda dansi na kurudi saa tisa kasorobo usiku.Hii si kawaida ya wanawake.Kulingana na tamaduni tabia za kutafuta anasa kama hizi ni kukosa maadili.
Mavazi ya Monika ni tofauti, anavaa surualili ilihili anafaa kujifunga kanga kama wanawake wengine.
Monika pia hali chakula cha jamii yake anasema ni kichafu.uk 13

Ushirikiano wa jamii
Katika jamii ya pale kijijini kuna ushirikiano wa hali ya juu.Uk Mhaji anamsaidia Keti Kutafuta pesa shilingi elfu tano.Hii ni baada ya yeye kukamatwa na polisi juu ya kesi yake na Asha.Mhaji wanamsaidia kwani ni mmoja wao.

Katika ri waya hii tunapata mahusiana mengi ya kijamii mfano, uk 57  Monika alikuwa amevunja ujirani,undugu na hisiani baina yao na Bi Riziki.Ni jamii ambayo imejikita katika kusaidiana na kushauriana na kuwatoa wenzao walio kwa matatizo.

Ndoa na mapenzi
Uk 217 Ndoa ya Muna na Hasani ilijaa ugomvi kwani Hasani hakutaka Muna atoke, avae vizuri au asome na hatoi pesa za matumizi.
Kuna ndoa ya Rashid na Salama,Ali na Sara Monika naShabani.
Ndoa zinazoonekana kama zimefaulu ni zile za wazazi wa Monika,Muna na Ali.

Unafiki
Hii ni hali ya kujifanya juwa ni rafiki ilihali ni adui. Hali ya kutokuwa mkweli. Mfano uk 102-104 Monika Alielezwa na Mheshimiwa Selemani waziri wa Kilimo kuwa Juma alikuwa tu dereva wake na hakufanya kazi Wizara ya Biashara. Juma ni mnafiki kwani alikuwa amemdanganya Monika.
Unafiki mwingine unahusisha Mheshimiwa Matata ambaye alimdanganya Monika kuwa atamuoa lakini anafanya harusi na msichana mwingine.
Urafiki
 Rafiki ni mtu anayependana na kuaminiana na mwingine..Katika riwaya hii kuna marafiki wa dhati ambao wanafaana sana. Mfano Bi riziki na Bi Tatu  na Keti na Mariyamu
Kuna marafiki ambao ni wadanganyifu.Mfano  uk 56 tunaelezwa kuwa urafiki baina ya Salama ulikuwa unafifia baada ya Monika kuanza kuishi na Rashid ambaye alikuwa amemposa Salama.

Pia katika uk55 Muna na Monika walikuwa marafiki lakini kukengeuka kwa Monika kunawatenganisha.Uk 34 tunawaona  Muna na Monika  ambapo Muna anoona monika kama sahani ya santuri iliyokwaruzika na sindano yake kukwama mahali.

Malezi mema
Katika riwaya hii wazazi wanawapa watoto wao malezi mema.Mfano Uk 97 Roho ya Bi inaaza kuwa na hofu na wasiwasi kwa kuwa hakupa habarizozote kuhusu Monika.Hii inaonyesha kuwa bado alikuwa na mapenzi kwa mwanawe. Pia Monika anaporejea kwao Mhaji anamtafutia mume .

Katika Uk 134 keti anamshauri Rashid jinsi la kutatua ‘tatizo la Monika.’Si kukuita kuja kukulaumu …kama unavyojua sisi ni wazee na wajibu weyu ni kuwaongoza watao wetu hasa tunapoona maisha yao yanaenda kombo’.

Ufisadi
Katika riwaya hii watu wanaojihusisha na mambo ya ufisadi ni Alison, Mheshimiwa.
Alison anamhonga Rashid ili apate kandarasi na wizara.
Uchunguzi wa Rashid anapofutwa Kazi.Msichana ambaya anatembea katika nchi mbalimbali.Msichana huyu anufisadi mwingi.

Falsafa ya mwandishi
Mwandishi analenga kuonyesha mkengeuko.Anamtumia Monika ambaye amekengeuka.Hafuati utamaduni na hana heshima.Kwa upande mwingine Muna amesoma lakini badao anfuata tamaduni za ndoa. Msimamo wake ni kuwa mtu akisoma bado anafaa kuwa na ustaarabu.
Nadharia
Mwandishi ametumia Nadharia kama vile Uhalisia Kwani matukio ni ya kawaida kama  vile ugomvi wa kunyumbani.Polisi kuja kwa keti na Mhaji kumtemebelea rafiki yake na Kuomba msamaha.Kuna. Ufeministi kwani Monika,Muna salama Asha na Keti ni wahusika wa kike ambao wamejikakamua maishani.Mwandishi amewatumia wahusika hawa kuonyesha jinsi wanawake wanaweza kujing’atua kutoka gereza la utamaduni.
Hitimisho
Mwandishi amefaulu kutumia mbinu kama vile dialojia na taswira kutoa maudhui.Kwa kutumia na kulinganisha Monika na Muna .Amefaulu kuonyesha athari za masomo katikaa jamii.Amejikita katika mkengeuko . Kwa kutumia nadharia ya uhalisia amefaulu kuonyesha nafasi ya ndoa katika jamii.
Chuo Kikuu cha Egerton
Jacqueline Kamau
A13/30196/08
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
Fasihi ,Lugha na Isimu
 KISW 411; Fasihi Linganishi
 Uchambuzi wa riwaya ya Mwisho wa Kosa
 Mhadhiri; Bw.Gacheiya
11/04/ 2012









PLOTI
Huwa ni mtiririko wa matukio katika kitabu.Riwaya hii ina sura Kumi. Muhtasari wa sura hizo ni kama ifuatavyo;

Riwaya inapoanza tunapata Salama nyumbani kwao akiwa anawaza kuhusu Monika na jinsi amebadilika kimawazo.Anakumbuka siku alipokuwa anatoka kazi na Bi Tatu akamuomba amsomee barua ya Monika.Monika aikuwa anawaarifu wazazi wake kuwa aalikuwa amefaulu na angerejea hivi karibuni. Siku inapowadia anakaribishwa na jamaa zake waliojaa fuha lakini yeye si mwenye furaha.

Monika anarejea kutoka ulaya alikokwenda kusoma. Waliokwenda kumlaki wanaonyeshwa dharau pale uwanja wa ndege.Tunaelezwa kuhusu kesi ya Asha na Bi keti  amabapo katika Uk 29 Keti anakamatwa na polisi na kesi yao kuanza.
Monika wanazozana na keti kuhusu uji.

Tunaelezwa mpango wa wazazi wa Ali juu ya ndoa ya Ali na Zabara uk 54Wazazi wake walimtarajia Ali aoe Zabara lakini Ali hakutaja lolote kuhusu ndoa kwa wazazi wake.Tunaelezwa jinsi ndugu na dadake zake Ali wanavyosumbuliwa na wasichana pale kijijini.

Monika na Muna wanakutana.Hawa ni wasichana wawili ambao wamesoma.Uk 55  kuna mazungumzo kati ya monika na Muna ambapo Monika anamuuliza Muna maswali juu ya ndoa yake.
Ugomvi baina ya Monika na Babake. Na Monika anaondoka kwao.Pia kuna ugomvi kati ya  Rashid na Monika wanapoishi pamoja.

Katika hii sura maudhui ya ufisadi yanajitokeza. Ufisadi kati ya Rashid na Alison.Ambapo Alison anapata kandarasi .Pia Mheshimiwa anataka kumhonga Rashid ili apate kandarasi pia.Tunaelezwa Kazi ya Rashid katika ofisi yake.

Monika anakutana na Mheshimiwa Selemani na kuuelewa unafiki wa Juma.
Tunaelezwa jinsi masomo ya Ali na jinsi madawaya kulevya yalimfanya afukuzwe shule.Uk 121 kuna barua ya kufukuzwa kwa Ali kutoka chuo kikuu.

Rashid anaenda kwa Saidi kupata ushauri,anahisi kuwa alikosea kwa kushiriki  ufisadi.Mhaji anamtemebelea Selele  na kumuomba amzungumzie Monika na amsaidie Monika kama mwanawe.Mhaji anataka monika aunganishwe na familia yake.

Karne anamsaidia Ali katika kazi yake mpya. Ali anapoenda kutafuta kazi ya kuandikia  anaelezwa na krani kuhusu kosa la shilingi 17,000 badala ya shilingi 1700.Hii ni hadithi ndani ya riwaya.

Kuna maelezo juu ya ndoa ya  Muna na Hasani ambayo imejaa matatizo.Hasani anamkataza Muna Kutoka au kusoma au kuenda kuwatembela wazazi wake.Muna ananyimwa uhuru na Mumewa ambaye pia hamtunzi vile mume anafaa kutunza bibi.

Ali anapata kazi mpya ofisini kwa Alison. Waziri Salimu anashindikizwa kumfuta kazi Rashid.Baadaye  Rashid anapata kazi katika kampuni ya Alison.
Uk 199 Monika anahama kwa Rashid  na kwenda kwa nyumba mypa aliyopewa ma Matata. Kuna ugomvi kati ya Matata na selemani kuhusu Monika.

Ndoa ya Hasani na Muna ambayo imejaa ugomvi inavunjika na Muna kurudi kwao.

Hasani anamuomba baba yake aende kuzungumza na wazazi wa muna anapoona Muna harudi Kwake. Baada ya kuzungumziwa na waazi wake Muna anarejea kwa mumewe na Hasani anaahidi kumtunza mke wake na kumpa uhuru wake.Ali hafurahishwi na uamuzi wa Muna lakini anakubali Shingo upande.

Kule Kazini Ali anaendelea vizuri na mafunzo yake na Alison anaahidi kumpeleka ngambo akasome zaidi.Ili aongeza maarifa katika kazi yake mpya.

Monika naye mambo yanamuendea kinyume.Matata haonekani na kuna fununu kwamba anaoa.Selemani anamueleza ukweli kuwa Matata alioa msichana wa miaka kumi na sita na anamushauri Monika arudi kwao. Selele anamusaidia kulipa kodi  na baadaye Monika anarudi kwao kwa masharti ya kutii na kusaidia pale nyumbani. Monika anarejea kwao na kuolewa na Shabani.

Selele anapanga karamu ya chakula cha mchana.Hapa walioshiriki wanazungumza jinsi maisha ya ulaya nay a Afrika yanatofautiana. Rashid anakuja na Salama,Monika na Shabani na Muna na Hasani. Ali na Sara wanapata kujuana na wazazi wanawasaidia kupanga kuoana. Riwaya inakamilka kwa ambayo iliandaliwa na Selele.



Ufisadi
Katika riwaya hii watu wanaojihusisha na mambo ya ufisadi ni Alison, Mheshimiwa.
Alison anamhonga Rashid ili apate kandarasi na wizara.
Uchunguzi wa Rashid unaochangia yeye kutwa Kazi kuna msichana ambaya anatembea katika nchi mbalimbali.Msichana huyu ana ufisadi mwingi.

Falsafa ya mwandishi
Mwandishi analenga kuonyesha mkengeuko.Anamtumia Monika ambaye amekengeuka.Hafuati utamaduni na hana heshima.Kwa upande mwingine Muna amesoma lakini badao anfuata tamaduni za ndoa. Msimamo wake ni kuwa mtu akisoma bado anafaa kuwa na ustaarabu.
Nadharia
Mwandishi ametumia Nadharia kama vile Uhalisia Kwani matukio ni ya kawaida kama  vile ugomvi wa kunyumbani.Polisi kuja kwa keti na Mhaji kumtemebelea rafiki yake na Kuomba msamaha.Kuna. Ufeministi kwani Monika,Muna salama Asha na Keti ni wahusika wa kike ambao wamejikakamua maishani.Mwandishi amewatumia wahusika hawa kuonyesha jinsi wanawake wanaweza kujing’atua kutoka gereza la utamaduni.
Hitimisho
Mwandishi amefaulu kutumia mbinu kama vile dialojia na taswira kutoa maudhui.Kwa kutumia na kulinganisha Monika na Muna .Amefaulu kuonyesha athari za masomo katikaa jamii.Amejikita katika mkengeuko . Kwa kutumia nadharia ya uhalisia amefaulu kuonyesha nafasi ya ndoa katika jamii.
MAREJELEO
1. Burhani Z.W.,(2004) Mwisho wa Kosa, LonghornPublishers (K) Ltd,Kenya.
2. Rocha M.Chimera, (1998) Kiswahili; Past, Present and Future Horizons,Nairobi University Press,.Nairobi

No comments:

Post a Comment

like it